NA MWANDISHI WETU - MTWARA.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuveri Homera, yuko mkoani Mtwara leo, Octoba 27, 2026 kwa ziara rasmi ya kikazi yenye lengo kuu la kutangaza rasmi ugunduzi mkubwa wa gesi asilia uliofanyika mkoani humo, hatua inayotarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa wananchi wa Mtwara, Lindi na Taifa kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Homera ameambatana na viongozi na wataalamu akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu pamoja na wajumbe wa kamati hiyo, wengine ni Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Mafuta na Gesi Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio, Menejimenti ya Wizara ya Nishati, pamoja na viongozi wa Bodi ya TPDC na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Akiwa mkoani Mtwara, Mhe. Waziri ameanza ziara yake kwa kufanya ziara na kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Kanali Donald Msengi.
Ziara hii inatajwa kuwa ya kimkakati katika kuhakikisha miradi mikubwa ya nishati, hususan gesi asilia na LNG, inawanufaisha wananchi moja kwa moja huku ikichochea kasi ya uwekezaji wa viwanda mkoani humo.








No comments:
Post a Comment