WIZARA YA MADINI YAWAKARIBISHA WADAU KUELEKEA UZINDUZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 28, 2026

WIZARA YA MADINI YAWAKARIBISHA WADAU KUELEKEA UZINDUZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA


Na Mwandishi Wetu - DODOMA


Waandishi wa habari, wahariri wa vyombo vya habari, wasanii, washawishi wa mitandao ya kijamii (*social influencers*) pamoja na wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini wametembelea ofisi za Wizara ya Madini zilizopo katika Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uzinduzi rasmi wa Mji huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 30, 2026.

Katika ziara hiyo, washiriki walipata fursa ya kutembelea ofisi za Wizara ya Madini na kutazama makala fupi iliyoelezea historia ya uanzishwaji wa Mji wa Serikali wa Mtumba, unaohudumia taasisi mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yake.

Uzinduzi wa Mji huo unatarajiwa kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye atakuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Ziara hiyo imelenga kuwapa washiriki fursa ya kuufahamu Mji wa Serikali wa Mtumba pamoja na kuelewa historia ya uanzishwaji wa Mji huo kuelekea uzinduzi wake rasmi.

No comments:

Post a Comment