AJALI YA NGUZO YA UMEME YASABABISHA GIZA MBEYA NA SONGWE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 21, 2026

AJALI YA NGUZO YA UMEME YASABABISHA GIZA MBEYA NA SONGWE


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kukatika kwa huduma ya umeme katika mikoa ya Mbeya na Songwe kufuatia ajali ya kuanguka kwa nguzo ya njia mpya ya kusafirisha umeme ya kilovoti 400 ya Mradi wa TAZA, eneo la Inyala mkoani Mbeya.

Ajali hiyo imesababisha kuharibika kwa miundombinu ya njia ya kusafirisha umeme ya kilovoti 220 inayosafirisha umeme kutoka Iringa kwenda Mbeya.

Kupitia taarifa iliyotolewa Jumamosi, Novemba 21, 2026, TANESCO imesema wataalamu wake tayari wamefika eneo la tukio na wanaendelea na kazi za ukarabati ili kurejesha huduma hiyo.

Hata hivyo, Shirika limeonya kuwa kutokana na ukubwa wa uharibifu, kurejea kwa huduma ya umeme kunaweza kuchelewa, huku likiahidi kuendelea kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya ukarabati.

TANESCO imewaomba wananchi wa mikoa hiyo kuwa na subira na kuomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.



No comments:

Post a Comment