Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) imezitaka kampuni za michezo ya kubahatisha (betting) na kasino, kuzingatia kikamilifu sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia sekta hiyo ili kulinda maadili na ustawi wa vijana, sambamba na kuongeza mchango wao katika maendeleo ya kijamii kupitia sekta za elimu, afya na michezo.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa GBT, James Mbalwe, wakati akiongoza hafla ya uzinduzi wa kampuni mpya ya michezo ya kubashiri ya Sasa Bet, iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuwazawadia wateja zawadi mbalimbali, ikiwemo gari jipya aina ya Jetour.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbalwe alisema ongezeko la kampuni zinazoendesha shughuli za michezo ya kubahatisha nchini linapaswa kwenda sambamba na manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa taifa, yakiwemo mapato ya Serikali na mchango katika kuboresha huduma za kijamii.
“Tunawakaribisha Sasa Bet katika soko la Tanzania. Tumeona wameanza vizuri kwa kuja na kampeni hii inayolenga kuwazawadia wateja wao zawadi mbalimbali, ikiwemo gari jipya la kisasa. Hata hivyo, tunatoa wito kwao na kampuni nyingine katika sekta hii kuongeza tija ya shughuli zao kwa kuhakikisha wanarejesha kwa jamii kupitia kusaidia sekta za afya, elimu, michezo na maeneo mengine muhimu ya maendeleo,” alisema Mbalwe.
Aidha, aliwataka washiriki wa michezo ya kubahatisha, hususan vijana, kushiriki kwa uwajibikaji na kwa kiasi, huku wakitambua umuhimu wa kutenga muda na rasilimali zao kwa ajili ya kazi, shughuli za uzalishaji na majukumu mengine ya kijamii.
Akizungumzia kampeni hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sasa Bet, Jimmy Kenneth, alisema kampeni hiyo itadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja na inajulikana kwa jina la “Kusanya Point, Usepe na Jetour”, ikiwa na lengo la kuwapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, kuanzia fedha taslimu kila wiki hadi gari jipya aina ya Jetour.
“Promosheni hii imeandaliwa mahususi kwa ajili ya wadau na wateja wetu. Kupitia kampeni hii, tutakuwa tukiwazawadia washindi 50 fedha taslimu kila wiki, huku zawadi kubwa ikiwa ni gari jipya aina ya Jetour litakalotolewa kila baada ya miezi mitatu,” alisema.
Aliongeza kuwa Sasa Bet imejipanga kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia sheria, kanuni, masharti na miongozo ya mamlaka zinazosimamia sekta ya michezo ya kubahatisha nchini, sambamba na kutekeleza wajibu wake kwa jamii kwa kushiriki katika kusaidia programu na shughuli mbalimbali za kijamii, hususan katika sekta za elimu, afya na michezo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), James Mbalwe (kushoto), sambamba na Mkurugenzi na Mmiliki wa Sasa Bet, Vakhtang Nikoleishvili (katikati), pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Jimmy Kenneth (kulia) wakijipongeza wakati wakionyesha zawadi ya gari jipya aina ya Jetour litakalotolewa kama zawadi kwa washindi wa kampeni ya Sasa Bet, kampuni mpya ya michezo ya kubashiri nchini. Kampeni hiyo inayojulikana kwa jina la “Kusanya Point, Usepe na Jetour” inawapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, zikiwemo fedha taslimu kwa washindi 50 kila wiki na gari jipya aina ya Jetour kila baada ya miezi mitatu.
Akizungumzia kampeni hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sasa Bet, Jimmy Kenneth (alieshika mic) alisema kampeni hiyo itadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja na inajulikana kwa jina la “Kusanya Point, Usepe na Jetour”, ikiwa na lengo la kuwapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, kuanzia fedha taslimu kila wiki hadi gari jipya aina ya Jetour.

No comments:
Post a Comment