Waziri wa Mambo ya Nje wa Usultani wa Oman, Mhe. Sayyid Badr bin Hamad bin Hamood Albusaidi, Novemba 9, 2026 amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mhe. Albusaidi amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo.












No comments:
Post a Comment