Zimepita siku chache tu toka Justin Bieber atangaze kuanza kwa tour yake ‘Purpose world tour ‘ mwanzoni wa mwaka 2016, tour itakayompeleka nchi 56 kwa ajili ya kuitangaza Album yake mpya, PURPOSE.
Licha ya ticket za tour hiyo kuuzwa bei ya juu, mitandao mingi Marekani imekuwa ikiripoti kasi ya ticket hizo kununuliwa huku wengine wakisema mwaka 2015 umeishia kuwa mwaka poa sana kwa Justin Bieber… Lakini kingine kikubwa cha kujua kuhusu tour hii ni package special ya VIP Selfie itakayopatikana kwenye tour ya Justin itakayoanza mwezi March mwaka 2016!
Kwa mujibu wa Altitude Tickets, package special ya VIP Selfie yani ‘I’ll Show You VIP #Purpose Experience’ itauzwa kwa USD $925 ambayo ni sawa na milion 1,850,000, na watu watakaonunua package hiyo wataweza kupiga picha moja tu (sio mbili wala tatu) ya pamoja (Group Selfie) na Justin Bieber na kushare na watu wao kwenye Instagram… cha kushangaza zaidi ni kwamba package hii ya ticket zimeshakwisha tayari, yani SOLD OUT!!
No comments:
Post a Comment