Klabu ya Real Madrid ya Hispania ndio klabu yenye rekodi ya kumiliki na kupenda kununua wachezaji wenye majina makubwa kwa kiasi kikubwa cha fedha, Madrid ambao hadi sasa ndio wanashikilia rekodi ya kununua wachezaji ghali zaidi duniani Gareth Bale na Cristiano Ronaldo wana utamaduni wa kipekee wa kuhakikisha wanampata kila mchezaji wanaomtaka.
November 20 stori kutoka katika mtandao wa dailymail.co.uk umeeleza kuwa miaka 10 iliyopita Real Madrid walitaka kumsajili Ronaldinho
ila muonekano wake sio mzuri hivyo asingefanya vizuri katika mauzo ya
jezi ya timu hiyo licha ya kuwa alikuwa na uwezo mkubwa na jina, Madrid waliachana na mpango wa kumsajili Ronaldinho na kumsajili David Beckham.
Stori kutoka dailymail.co.uk zinasema Fiorentino Perez
ambaye ndio alikuwa anahusika katika kukamilisha mpango huo anatajwa
kuwahi kukiri kuwa ni kweli walipanga kumsajilii staa huyo ila muonekano
wake ungeshusha brand yao, anasema nchi za Asia muonekano unasaidia sana kuongeza mauzo ya jezi ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza mapato kwa klabu.
Mwaka 2003 klabu ya FC Barcelona ilimsajili Ronaldinho na miaka miwili baadae akaingia katika headlines kwa kuwafunga wakiwa pamoja na David Beckham akiwa na uwezo ila moja kati ya sababu zilizowafanya wamsajili ni muonekano wake, katika mchezo huo Ronaldinho alifunga magoli mawili na Eto’o goli moja, lakini mchezo ulimalizika kwa Ronaldinho kuwa mchezaji bora wa mechi.
No comments:
Post a Comment