HUKU
Viongozi wa Spain wakiahidi ulinzi mkali Jumamosi Uwanjani Santiago
Bernabeu kwenye ule mtanange mkali kati ya Miamba ya La Liga Mabingwa
Barcelona na Real Madrid unaobatizwa 'El Clasico', stori ya mjini ni
kitendawili kama Supastaa Lionel Messi ataanza Mechi hii.
Ulinzi mkali umeahidiwa huko Bernabeu kufuatia hali tete ya usalama
huko Ulaya iliyosababisha Mechi kubwa kadhaa kufutwa kutokana na
vitisho kufuatia mauaji mabaya ya Watu 129 huko Paris Ijumaa iliyopita.
Jumamosi, ndani ya Bernabeu, kunatarajiwa kuwa na Washabiki 80,000
Vitini wakilindwa na Polisi na Wanausalama wengine idadi yao ikiwa
maradufu ya ile ya kawaida.
Kisoka, Mechi hii, mbali ya kuwa ni El Clasico, safari hii
inawakutanisha Barcelona, wanaaoongoza La Liga wakiwa Pointi 3 mbele, na
Real Madrid walio Nafasi ya Pili.
Lakini mvuto mkubwa Siku zote ni ile vita binafsi kati ya Mastaa wa
Klabu hizi mbili, Cristiano Ronaldo wa Real na Messi wa Barca.
Wakati Ronaldo yuko fiti na alipumzishwa na Nchi yake Portugal
kucheza Mechi za Kimataifa wakati Ligi imesimama kwa Wiki 2 huku
mwenyewe akijifua kivyake, Messi alikuwa nje ya Uwanja tangu Septemba 28
alipoumia Goti.
Lakini, kwa takriban Wiki moja sasa, Messi anerejea Mazoezini na
swali ni je Kocha wa Barca, Luis Enrique, atamuanzisha Mechi hii?
LA LIGA
RATIBA
**Saa za Bongo
Jumamosi Novemba 21
1800 Real Sociedad v Sevilla
2015 Real Madrid v Barcelona
2230 Espanyol v Malaga
0001 Valencia v Las Palmas
0005 Deportivo La Coruna v Celta de Vigo
Jumapili Novemba 22
1400 Sporting Gijon v Levante
1800 Villareal v Eibar
2015 Granada v Athletic Bilbao
2130 Real Betis v Athletic Madrid
Jumatatu Novemba 23
2130 Getafe v Rayo Vallecano
No comments:
Post a Comment