Ikiwa msimu wa mwaka 2015/2016 wa Ligi Kuu Uingereza unatajwa kuwa sio mzuri kwa kocha wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Jose Mourinho
kiasi cha jana kuvunja rekodi yake kwani hakuwahi kufungwa mechi saba
katika msimu mmoja wa Ligi Kuu, November 8 kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amekubali kikosi chake kitoke sare dhidi ya Tottenham Hotspurs.
Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani huku wakiwa na kumbukumbu kichwani ya kufungwa goli 5-1 na FC Bayern Munich katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hawakutaka kupoteza mchezo wa pili mfululizo hasa wakiwa katika dimba lao la Emirates, licha ya kuwa Arsenal wamekuwa wakipata matokeo mazuri msimu huu wameshindwa kuwafunga Spurs.
Arsenal waliokuwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza msimu huu nyuma ya Man City kwa tofauti ya point moja, wametoka sare ya goli 1-1 na vijana wa kocha Mauricio Pochettino, Tottenham walifanikiwa kupata goli la kuongoza dakika ya 32 kupitia kwa mshambuliaji ambaye inatajwa kuwa Arsenal waliwahi kumuacha enzi za utoto Harry Kane kabla ya beki wa Arsenal Kieran Gibbs kusawazisha goli hilo dakika ya 77.
Matokeo ya mechi za nyingine za Ligi Kuu Uingereza November 8
-
Aston Villa 0 – 0 Manchester City
-
Liverpool 1 – 2 Crystal Palace
No comments:
Post a Comment