Kivumbi cha Ligi Kuu Hispania kimeendelea tena Jumapili ya November 8 kwa michezo minne kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, klabu ya FC Barcelona ambayo bado inaendelea kumkosa staa wa kimataifa wa Argentina anayekipiga katika klabu hiyo Lionel Messi imeshuka dimbani kuwakabili Villarreal katika dimba la Nou Camp.
FC Barcelona wakiwa na washambuliaji wao mahiri Luis Suarez na Neymar na kumkosa Lionel Messi wamefanikiwa kubakiza point tatu muhimu katika uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp, FC Barcelona wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0.
Klabu hiyo ambayo haikufanikiwa kupata goli hata moja kipindi cha kwanza ilianza kupata goli la kwanza dakika ya 60 kupitia kwa Neymar kabla ya dakika 10 mbele Luis Suarez kufunga goli la pili kwa mkwaju wa penati, Barcelona waliamua kufanya mabadiliko dakika ya 79 na 82 ya kuwatoa Munir El Haddadi na Gerrard Pique na nafasi zao kuchukuliwa na Sandro Ramirez na Marc Bartra mabadiliko ambayo yaliendelea kuwa na uhai na Neymar dakika ya 85 akapachika goli la mwisho.
No comments:
Post a Comment