Michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na kati imeendelea tena November 25 kwa bingwa mtetezi wa Kombe hilo timu ya taifa ya Kenya kushuka dimbani kuchuana na timu ya taifa ya Burundi, huu ukiwa ni mchezo wa pili kwa timu hizo za Kundi B.
Mechi kati ya Kenya dhidi ya Burundi
ilikuwa ngumu kwani kila timu ilionekana kujipanga ili iweze kupata
ushindi mapema na kujihakikishia nafasi ya kutinga katika hatua ya robo
fainali ya michuano hiyo, Burundi ambao hawa rekodi ya kutwaa Kombe hilo kwa zaidi ya miaka 2o kwa mujibu wa takwimu za CECAFA walianza kupachika goli la mapema kupitia kwa mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe dakika ya 11.
Furaha ya Burundi ambao walikuwa na pont tatu kabla ya mchezo huu ilipotea baada ya dakika ya 30 toka Amissi Tambwe apachike goli la kwanza kwa timu yake ya taifa ya Burundi ila mshambuliaji wa Kenya Michael Olunga akapachika goli la kuisawazishia Kenya na kudhiirisha kuwa bado wanauwezo wa kutetea Ubingwa wao, hadi dakika 90 zinamalizika Kenya 1-1 Burundi.
No comments:
Post a Comment