Zlatan Ibrahimovic atakuwa nyumbani katika mji wa Malmo, Sweden wakati atakapokuwa na timu yake…lakini mashabiki wa nyumbani wameamua kuonyesha heshima kubwa kwake kwa kumkaribisha kwa staili ya aina yake ikiwa ni miaka 14 tangu aihame timu hiyo ya nyumbani.
Jengo refu kuliko yote katika mji huo wa Malmo umepambwa kwa herufi kubwa ya Z ikiwa na maana ya jina lake Zlatan.Hii ni moja ya ishara ya kumkaribisha tena staa huyo lakini safari hii akiwa na timu ya ugenini.
Zlatan amewaambia mashabiki wa Malmo wanaweza kuimba jina lake kama walivyokuwa wakifanya awali wakati akiitumikia timu hiyo.
Malmo ndiyo ilikuwa timu yake ya kwanza kubwa iliyomkuza kisoka kabla ya kununuliwa na Ajax ya Uholanzi.
No comments:
Post a Comment