Kwa sasa uongozi wa Simba uko katika harakati za
kutafuta wachezaji wapya kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi cha timu hiyo,
Kocha wa Simba, Dylan Kerr, sasa amekubali.
Kocha huyo amekiri kuwa Simba ilifanya makosa
kumuacha mshambuliaji Elias Maguli ambaye sasa anaitumikia Stand United.
“Nilifanya hivyo kwa sababu maalumu kwa ajili ya
kuhakikisha tunasajili wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa zaidi yake lakini
mambo yamekuwa tofauti.
“Maguli angeonyesha mapema uwezo wake kama
alionao sasa, hakika nisingependekeza atolewe, lilikuwa ni kosa kumuacha,”
alisema Kerr.
Tayari
Maguri ameifungia Stand United mabao 9 huku Simba ikiwa ina mabao 15 ya
kufunga katika kikosi chake chote. Upachikaji huo wa umemfanya Maguri
arejee katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ambacho sasa
kimeweka kambi nchini Afrika Kusini kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria,
Novemba 14.
No comments:
Post a Comment