Cristiano Ronaldo ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania
ameingia kwa mara nyingine katika headlines baada ya kutaja wachezaji
watano watakaofanya vizuri kwa miaka ya baadae yaani kuwa katika viwango
vya juu kama yeye na Lionel Messi.
Staa huyo ametaja list ya mastaa watano anaowakubali na anaamini watafika mbali katika soka, katika list hiyo Ronaldo amemtaja Memphis Depay wa Man United, Neymar wa FC Barcelona, Eden Hazard wa Chelsea, Paul Pogba wa Juventus na mchezaji chipukizi wa Real Madrid Martin Odegaard.
“Nimeona
wachezaji wengi wenye uwezo ila naweza wataja hawa Odegaard wa Real
Madrid ndio kwanza ana miaka 16 na Hazard lakini Memphis Depay wa Man
United pia ni mchezaji mzuri pamoja na Paul Pogba labda na
Neymar”>>> Cristiano Ronaldo
No comments:
Post a Comment