Ikiwa homa ya dirisha dogo la usajili inazidi kuchukua headlines Tanzania,
vilabu vikiendelea kusaka saini za wachezaji zinaowataka waongeze nguvu
vikisoni mwao kabla ya dirisha dogo la usajili halijafungwa December
15, nchini Uingereza homa ya dirisha dogo la usajili inazidi kuchukua headlines katika vilabu kadhaa ikiwemo Arsenal.
Kwa kiasi kikubwa klabu ya Arsenal inahusishwa kufanya usajili wa mchezaji au wachezaji wanafasi ya kiungo, Arsenal
kwa sasa ambayo inasumbuliwa na wachezaji wake kuwa majeruhi, hivyo
inahusishwa kwa karibu kutaka kusajili wachezaji wa nafasi ya kiungo
ambao ndio wengi wao majeruhi kikosi mwao.
Kwa sasa Arsenal ina wachezaji watano ambao ni majeruhi Aaron Ramsey, Francis Coquelin, Mikel Arteta, Jack Wilshere na Alex Oxlade-Chamberlain ila inahusishwa kutaka kuwasajili Luiz Gustavo, Christoph Kramer, Lucas Biglia, William Carvalho, Grzegorz Krychowiak, Cheikhou Kouyate, James McCarthy, Ever Banega na mkenya Victor Wanyama anayekipiga katika klabu ya Southampton ya Uingereza miongoni mwa majina hayo usishangae kama jina moja wapo likijiunga na Arsenal mwezi January.
No comments:
Post a Comment