Kuhusu Mwanamuziki Diamond Kuanza Kuimba Kingereza Kwenye Nyimbo zake Mpya... - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 24, 2015

Kuhusu Mwanamuziki Diamond Kuanza Kuimba Kingereza Kwenye Nyimbo zake Mpya...


Muziki ni lugha ya dunia, ndio sababu kuna wanamuziki wengi wanaimba lugha za kwao lakini bado wanafanya vizuri katika nchi nyingine zisizoongea lugha hizo.

Diamond Platnumz ametokea kuwa balozi mzuri wa lugha ya Kiswahili, kwasababu mafanikio aliyonayo sasa ya kufanya vizuri ndani na nje ya Afrika yametokana na nyimbo za Kiswahili alizotoa hadi sasa.

Baada ya kugundua kuwa kinachoweza kusababisha wimbo upendwe kimataifa sio lugha, hit maker huyo wa ‘Nana’ hana mpango kabisa wa kurekodi nyimbo za Kiingereza, licha ya kuwa ameshawahi kutoa wimbo wa Kiingereza, collabo yake na Iyanya ‘Bum Bum’ ambayo hata hivyo haikufanya vizuri kama nyimbo zake za Kiswahili.

“Hatuwazi kabisa kufanya nyimbo ya kizungu kwasababu Kiswahili ndicho kimetufanya tukavuka boda,” alisema Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond kupitia 255 ya XXL. “sio ushamba kutokuimba kizungu…Cabo Snoopy haimbi kizungu yule anaimba kikwao, wapo wakubwa kibao ambao wanaishi Ufaransa wanaimba Kifaransa wanaoishi Portugal wanaimba ki Portuguese, yaani hivyo, unatokea Tanzania imba Kiswahili, hata tukifika Nigeria wakimwona Diamond anafanya Interview ya kizungu wanamshangaa, wapo wanaokwenda pale hawajui hata kuongea kizungu…basi sometimes wanamuomba awafundishe maneno machache ya Kiswahili, ni dalili nzuri ya kutangaza lugha yetu.” alisema Tale.

Tale aliendelea kusema;

“Anayedharau asili yake hawezi kuvuka, tumekubalika kusikika Nigeria, Uganda wapi sehemu ambazo hazina Kiswahili kwasababu ya ‘Number 1 Remix’ ambayo Diamond aliimba Kiswahili mwanzo mwisho, na ‘Nasema Nawe’ imepata tuzo juzi Nigeria na ni ya Kiswahili typical. Kwahiyo tumesema si tunataka tupewe ubalozi wa kutangaza lugha yetu, na huwezi ukaimba kizungu R.Kelly akaimba kizungu halafu mkafananishwa, R.Kelly mwenye kizungu chake ndio ataonekana number One. Tukasema sisi haitatokea Diamond nyimbo hata moja kuimba kizungu na tunafanikiwa…Watu kibao waliwahi kuwaza huwezi kuwa International artist kama hujaimba kizungu, Diamond juzi ameshinda tuzo ile ya MTV Europe, hana nyimbo ya kizungu yoyote hana.” Alimaliza Babu Tale.

Msanii mwingine wa Afrika ambaye ameshaweka msimamo kuwa hatatumia kiingereza kwenye nyimbo zake ni rapper Sarkodie wa Ghana.

Sarkodie hutumia lugha ya kwao kwa kuchanganya na Kiingereza kidogo sana, lakini ni msanii ambaye ameshashinda tuzo mbalimbali kubwa kama ya BET Awards 2012 ‘Best International Act’, na ameshapata nominations za MTV MAMA, Channel O Music Awards, MOBO, AFRIMMA na zingine, kutokana na nyimbo hizo hizo.

No comments:

Post a Comment