MALINZI AWAPONGEZA SAMATTA NA ULIMWENGU...LEO ANAZINDUA KOMBE LA AZAM KARUME - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 9, 2015

MALINZI AWAPONGEZA SAMATTA NA ULIMWENGU...LEO ANAZINDUA KOMBE LA AZAM KARUME


RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu za pongezi wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kufuatia kutwaa Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) jana kwa kuifunga timu ya USM Algiers kwa jumla ya mabao 4-1.
Katika salamu zake kwenda kwa wachezaji hao, Malinzi amewapa hongera kwa mafanikio waliyofikia ya kutwaa ubingwa huo wa vilabu Afrika, na kuwataka waongeze bidii ili waweze kufanya vizuri pia katika michuano ya Kombe la Dunia la Mabara litakalofanyika mwezi Disemba nchini Japan.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (katikati) amewapongeza Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu baada ya kuipa TP Mazembe ubingwa wa Afrika 

Malinzi amesema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu na Watanzania wote wanawashukuru kwa kuiwakilisha vizuri Tanzania kimataifa, na sasa moyo huyo wa kujituma kwao waundeleleze katika mchezo dhidi ya Algeria wikiendi hii kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Wakati huo huo: Rais wa TFF, Jamal Malinzi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa michuano ya Kombe la Shirikisho (AzamHD Federation Cup) utakaofanyika leo Jumatatu, saa 9 kamili mchana katika uwanja wa Karume ambapo timu ya Abajalo FC itacheza dhidi ya Transit Camp zote za jijini Dar es salaam.
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi jana kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa Karume uliopo mjini Musoma, ambapo Vill Squad ya jijini Dar es salaam iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3- 1 dhidi ya timu ya JKT Rwamkoma ya mkoani Kagera.
Katika uwanja wa CCM Kirumba, Pamba FC ya jijini humo watakua wenyeji wa timu ya wachimba dhahabu kutoka mkoani Shinyanga, Bulyanhulu FC mchezo utakaoza saa 10:30 jioni.
Jumla ya timu 64 zinashiriki  michuano hiyo kutoka Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kuwania kutwaa ubingwa, ambapo Bingwa wa michuano AzamHD Federation Cup atapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.

No comments:

Post a Comment