Ushindi
wa ugenini unaipa Korongo nafasi nzuri ya kuingia hatua ya mwisho ya
mchujo baada ya mchezo wa marudiano Jumapili mjini Kampala, Uganda.
Wachezaji
wote wa Simba SC, beki Juuko Murushid na mshambuliaji wa Simba SC,
Hamisi Kizza wamecheza jioni ya leo Uwanja wa Kegue mjini Lome.
Juuko
alicheza dakika zote 90, wakati Kizza alianza mechi hiyo kabla ya
kumpisha Brian Umony dakika ya 56.
Beki wa Yanga SC, Vincent Bossou wa Togo alikuwa benchi kwa muda wote wa mchezo huo timu yake ikifungwa nyumbani.
Hamisi Kizza amecheza leo Uganda ikishinda 1-0 ugenini dhidi ya Togo |
Beki wa Yanga SC, Vincent Bossou wa Togo alikuwa benchi kwa muda wote wa mchezo huo timu yake ikifungwa nyumbani.
Timu
zote zilikutanisha makocha wa zamani wa klabu ya Yanga SC ya Dar es
Salaam, Togo ya Mbelgiji Tom Saintfiet na Uganda ya Mserbia, Milutin
Sredojevic ‘Micho’.
Burundi
imefungwa mabao 3-2 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya KOngo (DRC) katika
mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini
Urusi.
Mabao
ya Burundi yamefungwa na Cedric Amissi dakika ya 38 na 83, wakati ya
DRC yamefungwa na Yannick Bolasie Yala dakika ya tano, Firmin Ndombe
Mubele dakika za 86 na 88.
Bao
pekee la Naby Deco Keita dakika ya 27 limeipa Guinea ushindi wa 1-0
ugenini dhidi ya Namibia, wakati Benin imeshinda 2-1 nyumbani dhidi ya
Burkina Faso. Mabao ya Benin yamefungwa na Stephane Sessegnon kwa
penalti dakika ya 45 na ushei na Bello Issiaka Babatounde dakika ya 84,
wakati la Burkinabe limefungwa na Prejuce Niguimbe Nakoulma dakika ya
51.
Mechi
za jana, timu za kusini mwa Afrika, Msumbiji na Zambia jana zimepata
ushindi mwembamba wa 1-0 kila timu katika mechi za kwanza za Raundi ya
Pili kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi.
Bao la dakika ya 55 la Helder Pelembe limeipa Mambas (Nyoka) ushindi wa 1-0 dhidi ya Gabon Uwanja wa Zimpeto mjini Maputo.
Gabon
ilimkosa mshambuliaji wake nyota, Pierre-Emerick Aubameyang wa Borussia
Dortmund ya Ujerumani anayesumbuliwa na maumivu ya misuli – ambaye
ameifungia nchi yake mabao 22 katika mechi 20.
Kipa
wa Sudan, Akram El Hadi Salim na beki Ramadan Agab watabeba lawama kwa
pamoja kwa kuiruhusu Zambia kupata bao pekee kwa makosa yao.
Kila mmoja alimsubiri mwenzake aokoea mpira kwenye eneo la penalti na Kalengo akauwahi kuifungia timu yake Uwanja wa Karima.
Ushindi
huo unaiweka Zambia katika nafasi nzuri ya kufuzu katika hatua ya
mwisho wa mchujo baada ya mcheo wa marudiano mjini Ndola Jumapili.
Mechi
zaidi za kufuzu Kombe la Dunia zinatarajiwa kuendelea kesho na
keshokutwa. Tanzania itawakribisha Algeria Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
No comments:
Post a Comment