Ommy Dimpoz Atoa Sababu za Wasanii wa Tanzania Kutumia Models wa nje Kwenye Video Zao - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 13, 2015

Ommy Dimpoz Atoa Sababu za Wasanii wa Tanzania Kutumia Models wa nje Kwenye Video Zao


Ommy Dimpoz ni kati ya wasanii wa Bongo ambao wameshoot video zao kadhaa nje ya Tanzania kwa kutumia waongozaji pamoja na video models wa nje.

Wengi wanaamini upo uwezekano wa wasanii kuamua kusafiri na models kutoka nyumbani kama ambavyo husafiri na dancers wao kwenda kushoot video nje, lakini Ommy Dimpoz ana sababu za kwanini hushindwa kufanya hivyo.

Mara nyingi models wa nje wako proffesional wanaweza kucheza character zote ambazo wamepangiwa,” alisema Ommy Dimpoz kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

“huku unajua kidogo kuna scene ambazo mtu anatakiwa acheze lets say amevaa swimming costume, unajua huku kumpata msichana ambaye anaamua kujiachia hivyo ni wachache sana, hata kama ikitokea mnaweza mkajikuta msichana huyo huyo atatumika kwenye video za watu wote”. Alisema Ommy.

Ommy pia ameongeza sababu nyingine kuwa ni kupunguza gharama ya kusafiri na watu wengi zaidi.

Kikubwa ni kupunguza gharama, huko wako kibao utawakuta wengi sana, kwa hiyo ndo mana nasema hiyo nayo inachangia, pia ni vigumu kuondoka na watu wote kwenda nao kushoot nao nje, kwa sababu kule unawapata kwa bei rahisi alafu ukilipia video ina maana unalipia kila kitu”,

Siku chache zilizopita mwigizaji wa filamu za Bongo Jacqueline Wolper alihoji kupitia Instagram, kwanini wasanii wetu wanatumia zaidi models wa nje kwenye video zao (Ingia hapa)? Sina shaka Ommy Dimpoz amejibu swali la Wolper.

No comments:

Post a Comment