Rafiki wa karibu na Wolper aliyeomba hifadhi ya jina lake mwanzoni mwa wiki hii, aliliambia gazeti hili kuwa Wolper kwa sasa amekolea sana kwenye mambo ya siasa na kuona kama amekuwa akipoteza muda mwingi kwenye mambo ya uigizaji.
Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, mwandishi wetu alimtafuta Wolper ambaye alikiri kuamua kupumzika kidogo mambo ya uigizaji huku akishindwa kuweka wazi atajikita kwenye nafasi gani ndani ya ulingo wa kisiasa.
“Aah, kila mtu ana mipango na malengo yake, ni kweli kwa sasa nina mambo mengi ya kufanya kupitia siasa, nimejifunza vitu vingi mno vya msingi na muhimu, nimeweka kando kwa muda uigizaji, muda ukifika wa kuendelea na fani hiyo, nitasema,” alisema Wolper.
Source:Globalpublishers
No comments:
Post a Comment