MAJWEGA (KULIA) WAKATI AKIWA AZAM FC, AKIPAMBANA NA JUMA ABDUL WA YANGA. |
Taarifa
kwa vyombo vya habari
Simba
Sports Club
Dar
es salaam
18-11-2015
Klabu
ya Simba inapenda kuwafahamisha kuwa imeridhia ombi la kufanya mazoezi na timu
yetu toka kwa mchezaji wa kimataifa wa Uganda, Brian Majwega.
Ombi
hilo la Majwega limekuja kwetu ili apate kujiweka fit. Ukizingatia kazi rasmi ya
mchezaji huyo ni kucheza mpira wa miguu
Kwa
sasa mchezaji huyo ana mgogoro na klabu yake ya zamani timu ya Azam FC ya
jijini Dar es salaam
Katika
barua yake kwa klabu ya Simba ambayo nakala yake imetumwa shirikisho la mpira
wa miguu nchini TFF. Majwega ameomba kujumuika na timu yetu ukizingatia uwepo
wa wachezaji wengine wa kiganda Juuko Murshid na Hamis kiiza
Kesho
alhamis tarehe 19-11-2015 Majwega ataanza rasmi mazoezi na klabu yetu.chini ya
kocha Kerr jijini Dar es salaam
Imetolewa
na
Haji
S Manara
Mkuu
wa mawasiliano
Simba
sports club
Simba nguvu moja
No comments:
Post a Comment