Shambulizi la roketi dhidi ya Islamic State
Urusi
imesema kuwa imetekeleza shambulio kali zaidi dhidi ya maeneo
yanayokaliwa na wapiganaji wa Islamic State nchini Syria,ikiwa ni
miongoni mwa mashambulizi yake ya hewani kufikia sasa.
Waziri wa
ulinzi Sergei Shoigu,amethibitisha ripoti za Ufaransa na Marekani
kwamba Moscow ilitumia mabomu ya masafa marefu na makombora .
Amesema
kuwa ndege hiyo ilirusha makombora katika maeneo ya wapiganaji hao mjini
Raqqa,ambao ndio ngome kuu ya wapiganaji hao na Deir ez Zor mashariki
mwa Syria,huku mabomu yakilenga Kaskazini.
Awali
rais Vladmir Putin alionya mashambulizi makali dhidi ya IS,kufuatia
thibitisho kwamba ndege ya Urusi ilioanguka nchini Misri mwezi uliopita
ilisababishwa na shambulizi la kigaidi.
Maafisa wa Urusi wanasema kuwa chembechembe za vilipuzi zilionekana katika mabaki ya ndege hiyo aina Airbus.
Abiria wote 224 walioabiri ndege hiyo ,wengi wao wakiwa watalii wa Urusi waliuawa.
Kundi la Islamic State limethibitisha kutekeleza shambulio hilo.BBC
No comments:
Post a Comment