AFISA MTENDAJI MKUU WA GST AANZA KAZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, January 14, 2026

AFISA MTENDAJI MKUU WA GST AANZA KAZI


NA Mwandishi Wetu, Dodoma


Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Mhandisi Ally Samaje amewataka watumishi wa GST kufanya kazi kwa ushirikiano ili kukuza Sekta ya Madini hapa nchini kwani Taasisi hiyo ndio moyo wa Sekta hiyo.

Mhandisi Samaje ametoa wito huo leo Januari 14,2026 jijini Dodoma katika hafla ya makabidhiano ya ofisi pamoja na kikao alichofanya na watumishi wa GST ambapo amesisitiza watumishi kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuipeleka mbele Sekta ya Madini.

“Tufanye kazi kwa ushirikiano kama timu moja ili kuleta mageuzi katika sekta hii ya madini kwani taasisi hii ndio roho ya Sekta ya Madini” Amesema Mhandisi Samaje.

Aidha, Mhandisi Samaje amesema Taasisi hiyo ina kazi kubwa ya kufanya tafiti mbalimbali ambazo zitawawezesha wachimbaji wa madini wakubwa na wadogo kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kwa uhakika.

Sambamba na hayo, Mhandisi Samaje amesisitiza umuhimu wa Taasisi hiyo kuwa na vyanzo vya mapato vya uhakika ili kuwezesha shughuli za utendaji kazi pamoja na kuboresha maslahi ya watumishi.

“lazima tuangalie namna ya kuwa na _resources_ ambazo zitasaidia katika kutekeleza majukumu yetu vizuri samamba na kuboresha maslahi ya watumishi” Amesema Mhandisi Samaje.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa GST aliyemaliza mda wake Dkt. Mussa Budeba amemshukuru Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuamini kwa kipindi chote alichohudumu katika nafasi hiyo pamoja na watumishi wa GST kwa kufanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa.

Dkt. Budeba pia amewataka watumishi wa GST kumpa ushirikiano Afisa Mtendaji Mkuu Mpya pamoja na kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kukuza Sekta ya Madini.

“namshukuru sana Mhe. Rais kwa kuniamini kwa kipindi chote nilichohudumu kama Afisa Mtendaji Mkuu wa GST, pia nawashukuru viongozi wangu wa Wizara ya Madini kwa ushirikiano wao mkubwa walionipatia” Amesema Dkt. Budeba.

Naye mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya GST Bi. Yokbeth Myumbilwa akatumia nafasi hiyo kumuomba Afisa Mtendaji Mkuu Mpya kuendeleza yale yote mazuri ambayo atayakuta pamoja na kuwa na ubunifu na mambo mengine ambayo yatasidia kuipeleka mbele Taasisi hiyo.

“naomba endeleza vitu vyote vizuri vilivyoachwa na mtangulizi wako pamoja na kuongeza ubunifu wako mpya na kuangalia ni kwa namna gani unaweza kuongeza makusanyo ya taasisi” Amesema Bi. Myumbilwa

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Shughuli za Uendeshaji wa GST Bi. Neema Mhagama akizungumza kwa niaba ya Menejimenti na watumishi wa GST ameahidi kumpa ushirikiano Afisa Mtendaji Mkuu Mpya ili Taasisi hiyo ifikie malengo yake.

No comments:

Post a Comment