Bado headlines za usajili wa dirisha
dogo bado zinachukua nafasi kwa wachezaji kadhaa kuhusishwa kujiunga na
vilabu fulani na wengine kutemwa na vilabu vyao kutokana na
kutoridhishwa na viwango vya wachezaji hao. November 18 klabu ya Simba
imetangaza kuwatema wachezaji wawili wa kimataifa.
Simba ambayo ilikuwa inatajwa kwa karibu
kumtema Pape N’daw aliyetokea Senegal na mchezaji mmoja mwingine wa
kigeni, imethibitisha leo November 18 kuwatema wachezaji wawili Simon
Sserunkuma kutoka Uganda na Pape N’daw kutokea Senegal aliyeitumikia
klabu hiyo kwa nusu msimu na kocha wa Simba Dylan Kerr kupendekezwa
aachwe kutokana na kutoridhishwa na uwezo wake.
Kupitia kwa Afisa Habari wake Haji
Manara wametangaza kuwatema wachezaji hao na kumrejesha Paul Kiongera
aliyekuwa anaichezea KCB ya Kenya kwa mkopo. Hata hivyo mmoja kati ya
wanachama wa Simba amemleta mchezaji kutoka Cameroon Doumbie
Ernest usiku wa November 17 kwa ajili ya majaribio Simba.
“Simba
imeachana na Pape N’dawa na Simon Sserunkuma kutokana na mapendekezo ya
benchi la ufundi hususani mwalimu Kerr ila katika kuacha huko Simba
inamrejesha mchezaji wake Paul Kiongera aliyekuwa kwa mkopo KCB ya Kenya
na inaweza kusajili mchezaji mwingine
No comments:
Post a Comment