Diamond Platnumz na Patrick Ngowi kwenye list ya Waafrika 10 Mabalozi wa Tuzo za #TFAA2015 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 18, 2015

Diamond Platnumz na Patrick Ngowi kwenye list ya Waafrika 10 Mabalozi wa Tuzo za #TFAA2015



Najua ukianza kutaja list ya Tuzo ambazo mastaa wengi wamekuwa wakiingizwa kushiriki na kushindania, huenda jina la Tuzo za TFAA sio jina ambalo umelisikia mara kwa mara.
The Future Awards Africa (TFAA) ni Tuzo ambazo hutolewa kila mwaka kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18-31 waliofanya vizuri kwa kipindi cha mwaka husika, Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2004 na vijana wa Nigeria na mwaka 2015 zinatimiza miaka 10 ambapo kwenye list ya vijana waliotajwa kama Mabalozi waliowahi kushinda Tuzo hizo kwenye kipindi cha miaka 10, majina ya Watanzania wawili nayo yamo, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz na Patrick Ngowi.

No comments:

Post a Comment