Washambuliaji wawili wa TP Mazembe,
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanatarajia kutua jijini Dar es Salaam, leo.
Samatta
na Ulimwengu wataungana na Stars leo jioni kwa kuwa kikosi hicho
kinatarajia kutua jijini Dar es Salaam leo saa 12 jioni kikitokea Afrika
Kusini kilipoweka kambi ya zaidi ya wiki moja.
Samatta
na Ulimwengu walikuwa DR Congo ambako waliiongoza TP Mazembe kubeba
ubingwa wa Afrika na kuwa Watanzania wa kwanza kuvaa medali ya Ligi ya
Mabingwa Afrika.
Stars
utawasili hiyo jioni kwa ndege ya Fast Jet na moja kwa moja itakwenda
kambini kufanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mechi dhidi ya Algeria
itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.
No comments:
Post a Comment