TSHABALALA MCHEZAJI BORA WA MWEZI SIMBA SC - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 13, 2015

TSHABALALA MCHEZAJI BORA WA MWEZI SIMBA SC


BEKI wa kushoto wa Simba SC, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba katika klabu yake ya Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.

Tshabalala ameshinda tuzo hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi na mashabiki na wapenzi wa Simba kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.
Rais wa Simba SC, Evans Aveva ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE KWAMBA Tshabalala atakabidhiwa tuzo yake na zawadi baada ya kumaliza majukumu yake ya kitaifa. 
Mohammed Hussein 'Tshabalala' akimdhibiti kiungo wa Yanga SC, Deus Kaseke timu hizo zilipokutana katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwezi uliopita

Na Tshabalaa anakuwa mchezaji wa pili kushinda tuzo hiyo tangu Simba SC kuanzisha mpango huo, baada ya Mganda Hamisi Kizza kushinda mwezi Septemba. Kizza alishinda pia na tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwezi huo.
Tshabalala kwa sasa yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambacho kinajiandaa na mchezo wa Raundi ya pili kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria.
Taifa Stars itacheza na Algeria Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kurudiana Jumanne mjini Algiers na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya mwisho wa mchujo, ambayo itakuwa ya makundi katika mbio za Urusi 2018.

No comments:

Post a Comment