UHURU SELEMANI AKIZUNGUMZA NA FARID MUSSA ALIPOTEMBELEA KAMBI YA TAIFA STARS KWENYE HOTELI YA HOLIDAY INN EXPRESS JIJINI JOHANNESBURG. |
Kiungo
mshambuliaji wa Royal Eagles ya Afrika Kusini, Uhuru Selemani amesafiri
kilomita 568 kutoka jiji la Durban hadi Johannesburg nchini Afrika Afrika
Kusini, kwa ajili ya kuwaona na kuwasalimia wachezaji wa Taifa Stars walio
kambini.
Taifa
Stars imeweka kambi jijini Johannesburg kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria
kuwania kucheza Kombe la Dunia ambayo itapigwa Novemba 14 jijini Dar es Salaam.
Baada
ya kuwasili katika kambi ya Stars, Uhuru alionekana ni mwenye furaha, aliungana
na wachezaji, makocha na memba wengine wa benchi la ufundi la Stars.
Alikula
nao pamoja na kuzungumza nao hali iliyoonyesha kuchangamsha kambi.
“Nilitaka
kuja mapema, lakini nisingeweza kwa kuwa tulikuwa tuna mechi ya ligi jana.
Tumecheza na kushinda nashukuru.
“Nikaona
leo ni siku nzuri kuja kukutana na ndugu zangu. Nimejiona kama niko nyumbani.
“Kweli
ni mbali sana, lakini ilikuwa ni lazima nije na kuwaunga mkono ndugu zangu hapa
ambao wameweka kambi kulipigania taifa,” alisema Uhuru.
Uhuru
aliyewahi kuzichezea Simba, Coastal Union, Mtibwa Sugar na Azam FC, anatarajia
kurejea Durban kesho baada ya kukata kiu yake ya kuwaona wachezaji wa Stars,
wengi wao akiwa amewahi kucheza nao katika timu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment