Alhaj
Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ ameteuliwa kuwa kocha wa timu ya
Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars itakayoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika Mashariki na Kati.
Michuano
hiyo maarufu kama Cecafa Challenge 2015 itafanyika nchini Ethiopia na itaanza
kutimua vumbi kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 6 mwaka huu.
Kwa
sasa Kibadeni ni mshauri mkuu wa kiufundi katika kikosi cha Taifa Stars
kilichoweka kambi jijini Johannesburg, Afrika Kusini kujiandaa na mechi dhidi
ya Algeria, Novemba 14.
Tayari
makundi yametangazwa na Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi A pamoja na wenyeji
Ethiopia, Zambia na Somalia ambalo ni kundi humu.
Kundi B lina timu za Uganda, Burundi na Djibouti wakati Zanzibar iko Kundi C lenye timu za Sudan Kusini, Sudan na Rwanda.
No comments:
Post a Comment