ULINZI MKALI KAMBI YA TAIFA STARS SAUZ - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 6, 2015

ULINZI MKALI KAMBI YA TAIFA STARS SAUZ


KAMBI YA TAIFA STARS JIJINI JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI
 Johannesburg
KAMBI ya Taifa Stars iko katika hoteli ya Holiday Inn jijini hapa na ulinzi ni mkali hasa.

Mazingira ya kambi hiyo yako katika utulivu sana na uzio wote umezungushiwa nguzo za umeme.

Anayeingia lazima anahojiwa na askari zaidi ya wanne ambao wanakuwa kwenye lango kuu la kuingilia.
Hata akiingia analazimika kuyapita majengo matatu kabla ya kufikia hoteli iliyo.
Hakuna sehemu yoyote ya karibu kwa ajili ya vinywaji au mtu anaweza kwenda kutembelea, badala yake hata kama ni maji au mahitaji ya ziasa ya wachezaji angalau takribani kilomita 2 yanaweza kupatikana.
Mratibu wa Taifa Stars, Msafiri Mgoyi amesema wamefanya hivyo ili kuweza kufikia malengo.
“Hii ni timu ya taifa, suala la usalama ni la kwanza. Lakini tunaangalia utulivu pia na kuhakikisha wachezaji wanapumzika,” alisema.


Stars inajiandaa kuivaa Algeria Novemba 14 jijini Dar es Salaam katika harakati zake za kuwania kucheza Kombe la Dunia. Mechi ya marudiano itachezwa Novemba 17 jijini Algers.

No comments:

Post a Comment