Akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa mara ya kwanza, Rais Dk. John Pombe Magufuli, jana amesema moja
kati ya sekta atakazofanya nazo kazi kwa umakini ni michezo.
Magufuli alisema ameitaja sekta ya michezo kuwa
ni miongoni mwa zinazopaswa kutazamwa kwa kina kwani ni moja kati vitu
vinavyochangia maendeleo ya nchi.
Alisema atahakikisha sekta ya michezo
inaboreshwa vilivyo ili iweze kuwanufaisha wananchi kwa kuwaongezea kipato kama
ilivyo katika mataifa mengine duniani yaliyopiga hatua katika sekta hiyo.
“Yapo mambo mengi ya kuyaangalia na kuyafanyia
kazi katika kipindi cha utawala wangu, moja kati hayo ni pamoja na sekta ya
michezo na utamaduni.
“Tutahakikisha tunayafanyia kazi ili kuongeza
wigo wa ajira kwa maendeleo ya taifa letu,” alisema Magufuli katika hotuba yake
ya kuzindua rasmi bunge.
Kabla ya kuzindua bunge hilo, Magufuli alimuapisha Waziri Mkuu, Majaliwa Kasim Majaliwa asubuhi kwenye Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma. Majaliwa ni mwanamichezo na ana taaluma ya ualimu wa soka.
No comments:
Post a Comment