Walisema Hataweza Kuleta Mabadiliko Ndani ya Mfumo wa CCM, Sasa Wanadai Anatekeleza ilani yao - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 24, 2015

Walisema Hataweza Kuleta Mabadiliko Ndani ya Mfumo wa CCM, Sasa Wanadai Anatekeleza ilani yao



Hawa marafiki zetu wa upinzani kwa maoni yangu ni watu wa kutafuta tafuta sababu za kujitetea!
Wakati CCM inampitisha Magufuli kuwa mgombea urais, jamaa wakajaribu kuja na hoja kwamba hata aje malaika hataweza kuleta mabadiliko Kwasababu ya mfumo uliopo!!

Hoja yao ikawa Magufuli anafaa kuwa Raisi lakini mfumo ulio chini ya chama cha Mapinduzi utakuwa kikwazo kwake kuleta mabadiliko ambayo Magufuli alikuwa akiya nadi wakati wa kampeni! Ajabu ni kwamba hawakutuambia wakati ule kwamba mabadiliko aliyokuwa anayanadi Magufuli wakati wa kampeni yako kwenye ilani yao. Wao walichokiona na kutuaminisha wananchi ni kwamba ilani ya CCM iliweka mabadiliko ambayo Magufuli atashindwa kuyaleta akiwa ndani ya mfumo huu!!
Kichekesho sasa!!!

Baada ya wananchi kutokuwaamini wapinzani na kumuamini Magufuli na wakamchagua kuwa Raisi.
Na Magufuli huyo akaanza kuzifanyia kazi zile ahadi za mabadiliko alizozitoa wakati wa kampeni, wale jamaa wanarudi tena na hoja nyingine,
Eti Magufuli ameamua kuifuata ilani yao na kuiacha ilani ya CCM aliyoinadi!!!
Hivi hizi ni akili timamu kweli????
Wamesahau kwamba wakati Magufuli akiinadi hiyo ilani wakati wa kampeni, hao hao waliiona ni nzuri lakini wakajaribu kuwaaminisha watz kwamba Magufuli atashindwa kuitekeleza Kwasababu ya mfumo!!

Leo Magufuli anawaonyesha kwamba mfumo hauwezi kumzuia kuitekeleza ilani hiyo ya CCM na mabadiliko iliyoya ainisha, wanasema hayo unayo yafanya yako kwenye ilani yetu!!!!
Hivi mabadiliko Yale mliyo sema atashindwa kuyaleta Kwasababu ya mfumo ni yapi????
Magufuli amewathibitishia kwa vitendo kwamba siku zote mko wrong!!!!
Inabidi mfikirie tena!!!!

No comments:

Post a Comment