WADAU wa Soka la England Wiki hii watafurahia mchanganyiko wa Mechi za Ligi Kuu England na zile za Robo Fainali za EMIRATES FA CUP.
Kabumbu litaanza Ijumaa Usiku kwa Mechi ya Raundi ya 6 ya EMIRATES FA CUP, ambayo ndio Robo Fainali, kati ya Timu ya Daraja la chini na Timu ya Ligi Kuu England Crystal Palave ambao wako Ugenini.
Hapo Jumamosi zipo Mechi 3 za Ligi na moja mtanange mkali wa FA CUP huko Goodison Park kati ya
Everton na Chelsea.
Jumapili ipo Mechi 1 ya Ligi huko Villa Park wakati Timu ya mkiani Aston Villa ikiikaribisha Tottenham ambayo iko Nafasi ya Pili kwenye Ligi.
Jumapili pia zipo Mechi 2 za Robo Fainali ya FA CUP kwa Mabingwa Watetezi Arsenal kucheza kwao Emirates na Watford na huko Old Trafford ni Man United na West Ham.
ENGLAND – Ratiba Mechi za Wikiendi
**Saa za Bongo
Ijumaa Machi 11
EMIRATES FA CUP – Raundi ya 6 [Robo Fainali]
2255 Reading v Crystal Palace
Jumamosi Machi 12
LIGI KUU ENGLAND
1545 Norwich v Man City
1800 Bournemouth v Swansea
1800 Stoke v Southampton
EMIRATES FA CUP - Raundi ya 6 [Robo Fainali]
2030 Everton v Chelsea
Jumapili Machi 13
LIGI KUU ENGLAND
1900 Aston Villa v Tottenham
EMIRATES FA CUP - Raundi ya 6 [Robo Fainali]
1630 Arsenal v Watford
1900 Man United v West Ham
No comments:
Post a Comment