Serikali
za Tanzania na Uganda zinatarajia kuanzisha mradi wa uwekezaji wa
ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta unaolenga kuongeza pato la taifa na
uchumi wa nchi hizo.
Mradi huo unatarajia kugharimu kiasi cha Dola za Marekani bilioni nne na utekelezaji wake utaanza mwanzoni mwa mwaka 2017.
Kauli
hiyo imetolewa jana Jumatatu (Machi 28, 2016) Jijini Dar es salaam na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa
mkutano wake na wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini.
Prof.
Ntalikwa alizitaja fursa ambazo zitanufaisha taifa kuwa ni pamoja na
kodi zitakazolipwa, kuongezeka kwa wigo wa ajira kupitia miradi huo
pamoja na tenda mbalimbali zitakazotolewa wakati na baada ya kukamilika
kwa ujenzi wa mradi huo.
“Tanzania
ina kila sababu ya kupata mradi huo kwa kuwa ina uzoefu wa kuwa na
mabomba kama hayo manne nchini na tunajivunia bandari yetu ya Tanga
yenye kina kirefu kuliko bandari zote Afrika Mashariki” alisema Prof. Ntalikwa.
Prof. Ntalikwa alisema
kuwa mwitikio wa wafanyabishara wa sekta ya mafuta nchini ni mzuri na
kubainisha kuwa wanatarajia kusafiri kuelekea nchini Uganda kujionea
fursa mbalimbali zinazopatikana nchini humo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini Dkt. Gideon Kaunda alisema
kwa upande wao wataitumia vyema fursa ya uwekezaji katika ujenzi wa
mradi huo na kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais
Dkt. John Pombe Magufuli.
Imeandaliwa na Eleuteri Mangi-MAELEZO
No comments:
Post a Comment