Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ametengua
uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bi.
Juliet Kairuki kuanzia tarehe 24 Aprili mwaka huu.
Taarifa
iliyotolewa na kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Biashara na
Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, imesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya
rais Dkt. Magufuli kupata taarifa kuwa Mkurugenzi huyo alikua hachukui
mshahara wa serikali tangu alipoajiriwa mwaka 2013 jambo ambalo linazua
maswali mengi.
Aidha,
taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu huyo imeongeza kuwa endapo Bi.
Kairuki atakuwa tayari kuendelea kufanyakazi na Serikali ya Awamu ya
Tano atapangiwa kazi nyingine. Mchakato wa kumpata Mkuregenzi mpya
umeanza mara moja.
Kwa
mujibu wa Prof. Mkenda kwenye taarifa yake hiyo amesema Bw. Clifford
Katondo Tandali, atakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho
cha Uwekezaji nchini TIC.
No comments:
Post a Comment