UEFA CHAMPIONZ LIGI-NUSU FAINALI: ATLETI YAITUNGUA BAYERN HUKO VICENTE CALDERON! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, April 28, 2016

UEFA CHAMPIONZ LIGI-NUSU FAINALI: ATLETI YAITUNGUA BAYERN HUKO VICENTE CALDERON!

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Nusu Fainali
Mechi za Kwanza
Matokeo:
Jumanne Aprili 26
Manchester City 0 Real Madrid 0
Jumatano Aprili 27
Atletico Madrid 1 Bayern Munich 0
++++++++++++++++++++++++++
ATLETI-BAYERN-LEWADOWSKIAtletico Madrid na Bayern Munich zilicheza Jana Mechi yao ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Vicente Calderon Jijini Madrid na Bao la Dakika ya 11 la Saul Niguez limewapa Atletico ushindi wa 1-0.
Bayern walitawala Kipindi cha Pili na kukosa Mabao kupitia David Alaba ambae Shuti lake la Mita 35 lilipiga Posti na jaribio la Arturo Vidal kuokolewa.
Katika Kipindi hicho cha Pili, shambulio la nadra la Atletico lilishia kwa Fernando Torres kupiga Posti.
Timu hizi zitarudiana Nyumbani kwa Bayern, Allianz Arena, Jumanne ijayo kuamua Mshindi ambae atakutana na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine kati ya Manchester City na Real Madrid watakaocheza Fainali huko San Siro, Milan, Italy hapo Mei 28.
VIKOSI:
Atletico Madrid: Oblak; Juanfran, Giménez, Savić, Filipe Luís; Gabi, Fernández, Saúl Niguez [Parteyat 85'], Koke, Griezmann, Torres
Akiba: Moya, Jesus Gamez, Lucas, Oliver, Thomas, Correa, Vietto.
Bayern Munich: Neuer; Lahm, Martinez, Alaba, Bernat [Benatia 77'], Alonso; Costa, Vidal, Thiago [Müller 70'], Coman [Ribért 64']. Lewandowski
Akiba: Ulreich, Kimmich, Tasci, Benatia, Ribery, Muller, Gotze.
REFA: Mark Clattenburg (England)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Nusu Fainali
Mechi za Pili
**Saa 3 Dakika 45 Usiku
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Jumanne Mei 3
Bayern Munich v Atletico Madrid [0-1]
Jumatano Mei 4
Real Madrid v Manchester City [0-0]
Fainali
Jumamosi Mei 28
**Saa 3 Dakika 45 Usiku

No comments:

Post a Comment