ATLETICO FAINALI ULAYA: BAYERN YAIFUNGA ATLETICO LAKINI NJE KWA BAO LA UGENINI! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 4, 2016

ATLETICO FAINALI ULAYA: BAYERN YAIFUNGA ATLETICO LAKINI NJE KWA BAO LA UGENINI!

>>LEO BERNABEU NI REAL V CITY, NANI FAINALI NA ATLETI?

UEFA CHAMPIONZ LIGI
Nusu Fainali
Mechi za Pili
Jumanne Mei 3
**Kwenye Mabano Jumla ya Magoli kwa Mechi Mbili
Bayern Munich 2 Atletico Madrid 1 [2-2, Atletico wasonga kwa Bao la Ugenini]
Jumatano Mei 4
**Saa 3 Dakika 45 Usiku
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Real Madrid v Manchester City [0-0]
++++++++++++++++++++++++++
BAYERN2ATLETI1VIGOGO wa Germany Bayern Munich Jumanne Usiku wakiwa kwao Allianza Arena Mjini Munich wameifunga Atletico Madrid ya Spain Ba0 2-1 katika Mechi ya Pili ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini wametupwa nje kwa Bao la Ugenini na Atletico kutinga Fainali.
Wiki iliyopita huko Vicente Calderon Jijini Madrid Atletico walishinda 1-0 na hivyo Jumla ya Mabao kwa Mechi 2 kuwa 2-2 lakini Bao la Atletico katika kipigo chao cha 2-1 huko Allianz Arena limewanufaisha kwa kuhesabika Mawili.
Katika Mechi hii ya Marudiano, Bayern walitangulia kufunga kwa Frikiki ya Xabi Alonso na kisha katika Dakika ya 34 Thomas Muller wa Bayern akakosa Penati iliyochezwa na Kipa Jan Oblak.
Kisha Antoine Griezmann akaisawazishia Atletico lakini Robert Lewandowski akaipa Bayern uongozi wa Bao 2-1 kwa Bao la Kichwa na Atletico kukosa Penati iliyopigwa na Fernando Torres katika Dakika ya 84.
++++++++++++++++
MAGOLI:
Bayern Munich 2 
-Alonso 31'
-Lewandowski 74'   
Atletico Madrid 1
-Griezmann 53'
++++++++++++++++
Atletico wanatinga Fainali ya Klabu Ulaya huku mara mbili wakikosa Taji baada ya
Kufungwa na Bayern Mwaka 1974 na Miaka Miwili iliyopita kutwangwa na Mahasimu wao Real Madrid.
Kwenye Fainali ya Mwaka huu itakayochezwa huko San Siro Mjini Milan, Italy hapo Mei 28, Atletico watacheza na Mshindi kati ya Real Madrid na Manchester City wanaorudiana Leo Usiku wakiwa 0-0 kutoka Mechi ya Kwanza.
VIKOSI:
Bayern Munich: Neuer, Lahm, Boateng, Javi Martinez, Alaba, Alonso, Douglas Costa, Muller, Vidal, Ribery, Lewandowski.
Akiba: Ulreich, Tasci, Thiago, Rafinha, Gotze, Coman, Kimmich.
Atletico Madrid: Oblak, Juanfran, Godin, Gimenez, Filipe Luis, Saul, Gabi, Fernandez, Koke, Fernando Torres, Griezmann.
Akiba: Moya, Savic, Correa, Lucas, Carrasco, Thomas, Vietto.
REFA: Cüneyt Çakır (Turkey)
Fainali
Jumamosi Mei 28
**Saa 3 Dakika 45 Usiku
Atletico Madrid v Real Madrid/Manchester City

No comments:

Post a Comment