Kwenye tukio hilo, Huth alimvuta Nywele Fellaini na Kiungo huyo wa Man United kulipiza hapo hapo kwa kumpiga na kiwiko na vitendo hivyo havikuonwa na Refa Michael Oliver.
Wachezaji hao wamepewa hadi Jumatano Saa 2 Usiku, Saa za Bongo, kujibu Mashitaka yao.
Ikiwa watapatikana na hatia wapo hatarini kupata Kifungo cha Mechi 3 kila mmoja na hili litamaanisha Msimu wao wa Ligi ndio umekwisha.
Lakini kwa sababu Man United wamebakiza Mechi 3 za Ligi na Leicester 2 tu, Fellaini anaweza kucheza tena Msimu huu kwenye Fainali ya FA CUP hapo Mei 21 dhidi ya Crystal Palace.
No comments:
Post a Comment