UEFA CHAMPIONZ LIGI
Nusu Fainali
Mechi za Pili
**Saa 3 Dakika 45 Usiku
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Jumanne Mei 3
Bayern Munich v Atletico Madrid [0-1]
Jumatano Mei 4
Real Madrid v Manchester City [0-0]
++++++++++++++++++++++++++
Hii ni Mechi kabambe ambayo inaweza kwenda kokote kufuatia Sare yao ya 0-0 huko Etihad Wiki iliyopita.
Lakini safari hii Real wako kwao Santiago Bernabeu Jijini Madrid na
upo uwezekana mkubwa kwa Cristiano Ronaldo kuwemo dimbani baada ya
kuikosa Mechi kwanza kutokana na tatizo la Musuli za Mguuni.
Wachambuzi wanahisi kama Ronaldo yuko fiti na atacheza basi Real
tayari wana mguu mmoja kwenye Fainali huko San Siro Jijini Milan, Italy
hapo Mei 28.
Kwa Manchester City, hii ni Nusu Fainali yao ya kwanza kucheza
wakiwania kwenda Fainali kwa mara ya kabisa kitu ambacho kitakuwa zawadi
spesho kwa Meneja wao kutoka Chile Manuel Pellegrini ambae hiyo itakuwa
Mechi yake ya mwisho kwani City tayari washamsaini Antonio Conte kutoka
Italy kuwa Meneja wao mpya kwa Msimu ujao.
Hali za Timu
Real Madrid wamefungwa Mechi 1 tu ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu
nah ii ni ile ya 2-0 walipofungwa na VfL Wolfsburg katika Mechi ya
Kwanza ya Robo Fainali lakini katika Marudiano wakajibu 3-0 na Bao zote
kupigwa na Ronaldo.
Msimu huu kwenye Mashindano haya wameshinda Mechi 8, Sare 2 na
Kufungwa 1 huku wakishinda Mechi zao zote 5 walizocheza Santiago
Bernabeu.
Manchester City wao rekodi yao ya Mashindano haya Msimu huu ni
Ushindi 6, Sare 3 na Kufungwa 2 huku Mechi za Ugenini wakishinda 3, Sare
1 na Kufungwa 1.
Hali za Wachezaji
Real Madrid:
Cristiano Ronaldo hajawa fiti bado lakini yupo mazoezini na wenzake lakini kwa Karim Benzema upo wasiwasi mkubwa.
Manchester City:
Pigo kubwa kwa Manchester City ni kuumia kwa David Silva kwenye
Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali hii huko Etihad Wiki iliyopita na ni
maumivu ambayo yatamweka nje kwa Wiki 3.
Lakini pia upo wasiwasi wa kucheza Yaya Toure na Samir Nasri wote wakiwa na maumivu.
Uso kwa Uso:
Real Madrid hawajafungwa katika Mechi 3 walizocheza na Man City kwa
kushinda 3-2 huko Santiago Bernabeu na Sare 2 za 1-1 na 0-0 huko
Manchester.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Real Madrid (Mfumo 4-3-3):
Navas,
Marcelo, Ramos, Pepe, Carvajal,
Casemiro, Modric, Kroos,
Ronaldo, Bale, Benzema.
Manchester City (Mfumo 4-2-3-1):
Hart,
Kolarov, Otamendi, Kompany, Zabaleta,
Fernandinho, Fernando,
Sterling, De Bruyne, Navas,
Aguero.
REFA: Davir Skomina [Slovenia]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Fainali
Jumamosi Mei 28
**Saa 3 Dakika 45 Usiku
No comments:
Post a Comment