YANGA 'YAVUNJA STENDI SHINYANGA', PENGINE POINTI 3 TU MECHI 3 ZILOBAKI UBINGWA JANGWANI! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, May 3, 2016

YANGA 'YAVUNJA STENDI SHINYANGA', PENGINE POINTI 3 TU MECHI 3 ZILOBAKI UBINGWA JANGWANI!

LIGI KUU VODACOM                             
Matokeo:
Jumanne Mei 3
Stand United 1 Yanga 3

VPL-SIT-LOGO-1MABINGWA WATETEZI wa VPL, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, Yanga, Leo wameitandika Stand United Bao 3-1 huko Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na kujiwekea njia nyeupe kutwaa Ubingwa wao wa 27 ikiwa ni rekodi kwa Tanzania., Dakika za 2 na 45, na Amisi Tambwe, Dakika ya 63 wakati la Stand United lilikuwa la Penati ya Dakika ya 81 ya Elias Maguri.
Bao za Leo za Yanga zilifungwa na Donald Ngoma
Yanga sasa wamebakiza Mechi 3 tu za VPL na wana Pointi 68 wakifuatiwa na Azam FC wenye Pointi 59 na Simba Pointi 58 huku Timu hizo zikibakisha Mechi 4.
Hiyo inamaanisha ikiwa Azam FC watashinda Mechi zao zote zilizobaki wanaweza kufikisha Pointi  71 na Simba Pointi 70 lakini Yanga wakishinda Mechi 1 tu kati ya 3 zao zilizobaki watakuwa na Pointi 71 na ukichukulia Ubora wao wa Magoli basi huenda Yanga akatwaa Ubingwa kwa Pointi hizo 3 tu.
Hadi sasa Yanga ana Goli za Kufunga 64 Kafungwa 16 Tofauti ni 48 wakati Azam FC Kafunga 43 Kafungwa 16 Tofauti ni 27.
Yanga wamebakisha Mechi zote Ugenini dhidi ya Mbeya City, Ndanda FC na Majimaji FC.
LIGI KUU VODACOM
MSIMAMO:
VPL-MEI3
**Kwa hisani ya ‘NAIPENDA YANGA’
RATIBA:                                                
Jumatano Mei 4
Azam FC v JKT Ruvu
Jumamosi Mei 7
JKT Ruvu v Ndanda FC
Stand United v Coastal Union
Mgambo JKT v Mtibwa Sugar
Jumapili Mei 8
Tanzania Prisons v Majimaji
Simba v Mwadui FC
Kagera Sugar v Azam FC
Jumanne Mei 10
Mbeya City v Yanga
Jumatano Me 11
Majimaji v Simba
Jumamosi Mei 14
Mgambo JKT v JKT Ruvu
Ndanda FC v Yanga
Jumapili Mei 15
Mtibwa Sugar v Simba
Kagera Sugar v Stand United
Mwadui FC v Mbeya City

No comments:

Post a Comment