Mgeni
rasmi katika kilele cha maadhimisho ya mwaka huu ni Mheshimiwa Jaji
Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman. Wageni wengine mashuhuri
watakaohudhuria maadhimisho hayo ni pamoja na Waziri wa Habari, Michezo,
Utamaduni na Wasanii, Mhe. Nape Nnauye (mbunge), Mratibu Mkazi wa Umoja
wa Mataifa, mh. Alvaro Rodriguez, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) mh.
Roeland van de Geer, Mwakilishi Mkazi wa UNESCO Zulmira Rodrigues.
Wengine
ni watu mashuhuri mbalimbali kutoka Serikalini, wawakilishi wa
Mashirika ya Kimataifa na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania
wamethibitisha kushiriki. Wengine ni pamoja na watendaji wa vyombo vya
habari, Wabunge, wakuu wa Taasisi za kitaifa zisizo za Kiserikali, Vyuo
vya Uandishi wa Habari, wajumbe wa asasi za kiraia, waandishi wa habari
wakongwe.
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ni tukio kubwa la mwaka kwa vyombo vya habari na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kupata taarifa ni haki yako ya msingi: Idai”.
Wakati
wa maadhimisho haya, tunakumbuka gharama ambayo watu binafsi wanalipa
kwa kutoa habari, na kuwakumbuka kwa namna ya pekee watu hao ambao
wakati mwingine kwa kutoa kwao habari wanahatarisha maisha yao na kuweka
hatarini uhuru wao wenyewe, ili sisi tuweze kupata habari vizuri na
kuufahamu ukweli.
Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, inayoadhimishwa Mei 3 kila mwaka
duniani kote, ilianzishwa na Umoja wa Mataifa kusherehekea kanuni za
uhuru wa habari na kuwakumbuka wale waliokufa wakati wakijaribu
kutekeleza kanuni hizo. Siku hii hutumika kama jukwaa ambalo hutumiwa na
wadau wa vyombo vya habari kushinikiza mataifa kutengeneza sheria
rafiki za vyombo vya habari zinazoweza huhakikisha uhuru wa habari
katika nchi zao.
Maadhimisho ya siku hii kwa mwaka huu wa 2016, yanaadhimishwa sawia na matukio muhimu matatu ya kihistoria:
• Maadhimisho ya miaka 250 sheria ya kwanza ya uhuru wa habari duniani, ikijumuisha nchi za sasa za Sweden na Finland.
• Maadhimisho ya miaka 25 ya kupitishwa kwa Azimio la Windhoek Azimio la kanuni ya uhuru wa habari.
• Mwaka 2016 pia ni mwaka wa kwanza wa mzunguko wa miaka 15 wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Kutokana
na hali hii, Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa mwaka 2016
inaonyesha uhusiano kati ya uhuru wa habari, utamaduni wa uwazi na haki
ya uhuru wa habari, na maendeleo endelevu katika wakati wa digitali.
Jambo muhimu katika haya yote ni jukumu la msingi kwa waandishi wa
habari, na umuhimu wa kuwalinda wale ambao huleta huduma hii kwa umma.
Mkutano
huo pia utatoa nafasi ya kujadili na kushauriana kuhusu maana ya sheria
ambazo serikali imezipitisha na kuwasilishwa kwa mara ya kwanza katika
Bunge mwaka jana. Zinajumuisha Sheria ya Makosa ya Mtandao, Sheria ya
Takwimu, Muswada wa Huduma ya Habari na Sheria ya Upatikanaji wa Habari.
Wakati
wa tukio hilo waathirika wa ukiukwaji wa uhuru wa habari watatoa
ushuhuda juu ya changamoto walizokabiliana nazo wakati wa utekelezaji wa
majukumu yao.
Taarifa
kuhusu ya hali ya vyombo vya habari katika Kusini mwa Afrika
iliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika - MISA
inayojulikana kama Je Hii ni Demokrasia? itazinduliwa sambamba na Sera ya Jinsia kwa Vyombo Vya Habari vya Jamii.
Maadhimisho haya yanatarajiwa kuhudhuriwa na wadau wasiopungua 250, wa hapa nchini.
Maadhimisho
haya yameandaliwa kwa pamoja na MISA-Tanzania, UNESCO, Baraza la Habari
Tanzania (MCT), Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Umoja wa
Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Umoja wa Mataifa Ofisi ya
Tanzania, Taasisi ya Konrad-Adenauer-Stiftung Tanzania (KAS), Chama cha
Wamiliki wa Habari Tanzania (MOAT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Klabu ya
Waandishi wa Habari Mwanza na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
No comments:
Post a Comment