Katika
kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi ya kutamba nchini, makamanda wa
Polisi wa mikoa, wakuu wa upelelezi na waendesha mashtaka wameazimia
kuboresha ushirikiano wao katika kufanikisha kesi za wahalifu pindi
zinapofikishwa mahakamani ili waweze kupewa adhabu kali kwa mujibu wa
sheria.
Hayo
yamo katika maazimio ya watendaji hao wa haki jinai nchini katika kikao
kazi cha siku mbili kilichofanyika mkoani Dodoma na kuwashirikisha
makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa mikoa na wakuu wa
upelelezi wa mikoa.
Kikao
hicho kilikuwa chini ya uenyekiti wake Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP
Ernest Mangu pia kilihudhuliwa na mkurugenzi wa Mashtaka nchini, DPP
Biswalo Mganga, Makamishina wa Polisi, pamoja na taasisi mbalimbali
zinazohusika na upelelezi na uendeshaji wa mashtaka.
Wapelelezi
hao na waendesha mashtka walisema wataendeleza program za mafunzo ya
pamoja katika ngazi ya mkoa, kufanya vikao vya mara kwa mara ili
kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuendana na kasi ya
Serikali ya awamu ya tano lengo likiwa kuharakisha upelelezi na kutoa
haki kwa watuhumiwa.
Aidha,
wajumbe hao wa haki jinai wameazimia pia kukabiliana na changamoto ya
ucheleweshaji wa upelelezi wa kesi ambapo wamekubaliana kwa pamoja
kuzifikisha mahakamani kesi zote zenye ushahidi wa moja kwa moja ili
kuondokana na kesi kuchua muda mrefu na kuleta malalamiko kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment