CAF: DAU LA WASHINDI, WASHIRIKI MICHUANO AFRIKA LAPANDA, CHANGAMOTO KWA YANGA, SIMBA, AZAM!! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 10, 2016

CAF: DAU LA WASHINDI, WASHIRIKI MICHUANO AFRIKA LAPANDA, CHANGAMOTO KWA YANGA, SIMBA, AZAM!!



KUANZIA Mwaka 2017, Mashindano yote ya CAF Barani Afrika yatakuwa na Fedha nyingi zaidi kwa Washiriki na Washindi wake.

Tangazo hili la CAF, Shirikisho la Soka Barani Afrika, limekuja tu mara baada yao kusaini Mkataba na Kampuni ya Mafuta ya France TOTAL ambao unao thamani ya zaidi ya Dola Bilioni 1.

Hivyo Washindi wa AFCON, Kombe la Mataifa ya Afrika, watazoa Dola Milioni 4 kutoka Dola 1.5 ambazpo walipewa Mabingwa wa AFCON 2015 Ivory Coast.

Mabingwa wa CC, CAF CHAMPIONZ LIGI watazoa Dola Milioni 2.5 ikipanda toka Dola Milioni 1.5 walizopata hivi Juzi Klabu ya South Afrika Mamelodi Sundowns kwa kutwaa Ubingwa wa Afrika.

Kwenye Mashindano ya CL, CAF ya Kombe la Shirikisho, Mshindi sasa ataondoka na Dola Milioni 1.25 kutoka Dola 660,000 walizozoa TP Mazembe hivi Juzi.
Zawadi kwa Timu zinazotinga Hatua ya Makundi ya CC na CL zitapanda pamoja na Timu kuongezwa Hatua hiyo kutoka 8 kuwa 16.

Mshindi wa CAF super Cup atapewa Dola 100,000 ikiwa ni ongezeko la Asilimia 33.3 wakati Mshindi wa CHAN, Kombe la Mataifa ya Waafrika kwa Wachezaji wa ndani ya Afrika sasa atapa Dola 1.25 kutoka Dola 500,000 za sasa.

Bilas haka ongezeko hili la Bingo hii ni changamoto kubwa kwa Klabu zetu za Tanzania, Yanga, Simba na Azam FC, na wengineo kupigana vikumbo humu Bongo kusaka Mataji ili kucheza Klabu Afrika na kuzoa Fedha hizo bwelele.

No comments:

Post a Comment