KOEMAN AMTAKA MCHEZAJI WAKE ROMELU LUKAKU AHAME EVERTON AENDE KUNAKOSTAHILI KIPAJI CHAKE! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 10, 2016

KOEMAN AMTAKA MCHEZAJI WAKE ROMELU LUKAKU AHAME EVERTON AENDE KUNAKOSTAHILI KIPAJI CHAKE!


MENEJA wa Everton Ronald Koeman anaamini Romelu Lukaku anapoteza muda Klabuni hapo na anapaswa kuhama aende kunakostahili kipaji chake.

Koeman, Nyota wa zamani wa Netherlands, amekiri hana hakika kama Lukaku, Mchezaji kutoka Belgium mwenye Miaka 23, atabaki Everton Msimu ujao.
Mwanzoni mwa Msimu huu, Lukaku aliomba kuhama Everton lakini akabembelezwa kubaki kwa Msimu mmoja.

Koeman anaamini, Lukaku ambae amepachika Bao 7 kati ya Mechi zake 11 kwa Everton Msimu huu, anao uwezo wa kuichezea FC Barcelona Klabu ambayo ndio inasifika ni Bora Duniani.
Koeman ameeleza: “Nilimwezesha kujiamini na mwenyewe ametambua ni safi kwake kubaki Everton kwa Msimu mmoja ili ajiendeleze zaidi.”
Koeman ametoboa kuwa kipaji cha Lukaku ni kikubwa mno na si cha kumbakisha Everton milele.
+++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Romelu Lukaku alijiunga na Everton kwa Mkopo kutoka Chelsea Mwaka 2013 na kisha kusaini Mkataba wa kudumu kuanzia 2014 unaoisha 2019.
-Akiwa na Everton amefunga Bao 68 katika Mechi 137.
-Katika Ligi Kuu England, Lukaku ameifungia Everton Bao 50 na kumuweka kuwa Mfungaji Bora wa 3 kwenye Ligi hiyo katika Historia ya Everton akiwa nyuma ya Tim Cahill, Bao 56, na Duncan Ferguson, Bao 60.
+++++++++++++++++++++
Koeman amenena: “Patrick Kluivert pia alikuwa Straika na aliibuka bado Kijana tu na kuwa na Maisha safi Kisoka. Hatimae Kluivert akaichezea Barcelona na hili linawezekana kwa Lukaku!”

Aliongeza: “Bado ni Kijana sana lakini Lukaku ni Straika kamili. Anaweza kumiliki Mpira na pia kuwa ndie Straika pekee anaelengwa na Mipira kwa sababu ni mrefu na ana nguvu sana. Unaweza ukamtumbukizia Pasi ya Mipira mirefu toka nyuma na akaidhibiti!”

No comments:

Post a Comment