Jeshi la polisi nchini limesema litafanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa dhidi ya Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro na baadhi ya makamanda wa mikoa akiwemo kamanda wa mkoa wa Kinondoni Susan Kaganda.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai, CP Robert Boaz katika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
Kauli
hiyo ya CP Boaz kwa niaba ya jeshi la polisi imetolewa baada ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hivi karibuni kuwatuhumu makamanda
hao kuwa wanasita kuwachukulia hatua watumiaji na wauzaji wa kilevi cha
shisha kwa madai kuwa huenda wakawa wamepokea rushwa kutoka kwa
wanaojishughulisha na biashara hiyo.
Makonda alitoa
tuhuma hizo licha ya yeye ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama
katika kanda hiyo kutoa maagizo wahusika kuchukuliwa hatua.
CP Boaz alisema,
kuhusu tuhuma ya rushwa suala hilo lina taasisi zake zinazohusika, na
kwamba jeshi hilo limepokea tuhuma hizo dhidi ya askari wao kwa hiyo
watazichunguza kubaini ukweli.
No comments:
Post a Comment