LEO
huko Old Trafford Jijini Manchester, upo mtanange unaongojewa kwa hamu
na Mashabiki wengi wakati Manchester United wakukumbana na Arsenal
katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Mbali ya Mechi hii kukutanisha Vigogo wa EPL, mvuto mwingine mkubwa
ni kupambana uso kwa uso kwa Mameneja wa Timu hizo, Arsene Wenger wa
Arsenal na Jose Mourinho wa Man United, Mameneja ambao ‘hawapendani’ na
washakwaruzana sana wakati Mourinho akiwa na Chelsea.
Lakini hii itakuwa ni mara yao ya kwanza kuvaana tangu Mourinho awe Meneja Mpya wa Manchester United.
Hata hivyo, Juzi Wenger alisema tripu hiyo ya Arsenal huko Old Trafford ni Gemu tu kati ya Klabu mbili na si Mameneja Wawili.
Akiongea na Wanahabari hii hiyo Juzi, Wenger ameeleza: “Sidhani
kama napaswa kuelezea uhusiano wetu. Yeye atapigania Timu yake na mimi
nitapigania yangu. Hicho ni kitu cha kawaida!”
Aliongeza: “Siweki Gemu hizi kama ni Mashindano kati ya Mameneja
Wawili. Najua Watu wanataka kutengeneza uhasama lakini hilo halileti
Washabiki. Kitu ambacho kinavuta Washabiki ni Gemu yenyewe na ubora
wake. Ni muhimu iwe Gemu ya hali ya juu ili kuijengea sifa Ligi Kuu.
Hilo ni juu ya Wachezaji Uwanjani.”
Alipoulizwa kama atapeana mkono na Mourinho, Wenger alijibu huku
akitabasamu: “Ni wazi kitu hicho. Naheshimu utamaduni huo kwenye Ligi
Kuu.”
++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Mourinho na Wenger washapambana mara 14 kwenye Ligi Kuu England na Wenger hajashinda hata Mechi 1.
-Mourinho, akiwa na Chelsea, ameibuka Mshindi mara 8 na Sare 6.
-Mara pekee kwa Wenger kumbwaga Mourinho ni Agosti 2015 kwenye Mechi ya kugombea Ngao ya Jamii.
Kwenye Mechi hii ya Jumamosi, Man United itamkosa Straika wao
Zlatan Ibrahimovic ambae yupo Kifungoni Mechi 1 baada ya Kadi za Njano 5
lakini Wenger amemnyooshea kidole Kinda Marcus Rashford ambae kwenye
Mechi ya mwisho kati yao, Mwezi Februari, alifunga Bao 2 wakati Man
United inaichapa Arsenal 3-2 na kuing’oa kwenye Reli ya kusaka Ubingwa
Msimu uliopita.
Wenger amesema: “Mtu alietuua sisi ni Rashford. Hivyo tusidhanie
udhaifu wa Man United! Msimu uliopita tulipoteza Gemu 1 tu ya Ugenini,
huko Old Trafford. Na hiyo ilikuwa Gemu muhimu kwetu na tukapoteza
mwelekeo!”
JE WAJUA?
-Tangu Ligi Kuu England ianzishwe Msimu wa 1992/3, Arsenal wameshinda mara 3 tu Old Trafford katika Mechi 24.
Baada ya Mechi 11, Liverpool ndio Vinara wakiwa na Pointi 26,
Chelsea ni wa Pili wana 25, wakifuata Man City na Arsenal wenye 24 kila
mmoja, Tottenham wa 5 wakiwa na 21 na Man United ni wa 6 na wana 18.
Katika Mechi zao za mwisho za EPL kabla hawajapisha Mechi za
Kimataifa, Arsenal walitoka 1-1 na Tottenham katika Dabi ya London
Kaskazini na Man United kuitandika Swansea 3-1 huko Liberty Stadium,
Wales.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
MAN UNITED: De Gea, Darmian, Jones. Rojo, Shaw, Herrera, Pogba, Mata, Rooney, Martial, Rashford
ARSENAL: Cech, Jenkinson, Mustafi, Koscielny, Monreal, Coquelin, Xhaka, Ramsey, Ozil, Iwobi, Sanchez
REFA: ANDRE MARRINER
EPL - LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumamosi Novemba 19
1530 Manchester United v Arsenal FC
1800 Everton FC v Swansea City
Southampton FC v Liverpool
Sunderland v Hull City
Watford v Leicester City
Crystal Palace FC v Manchester City
Stoke City FC v Bournemouth FC
2030 Tottenham Hotspur v West Ham United
Jumapili Novemba 20
1900 Middlesbrough v Chelsea FC
Jumatatu Novemba 21
2300 West Bromwich Albion FC v Burnley FC
No comments:
Post a Comment