 |
| Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza mara baada ya kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. |
 |
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kuzungumza na Watumishi wa Zahanati ya Mihama na Wananchi wa Mihama wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati hiyo uliotekelezwa na TASAF iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
|
 |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt, Damas Ndumbaro wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama uliotekelezwa na TASAF iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
|
 |
Sehemu ya Wauguzi na Maafisa Tabibu wa Zahanati ya Mihama wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya Mwenyekiti huyo na Kamati yake kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
|
 |
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakikagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. Wengine ni Viongozi wa Mkoa wa Mwanza, Watendaji wa TASAF na Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo.
|
 |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa TASAF, Bw. Shadrack Mziray (kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama uliotekelezwa na TASAF iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
|
 |
Sehemu ya Wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya Mwenyekiti huyo na Kamati yake kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
|
 |
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Zahanati ya Mihama wakati wa ziara ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati hiyo uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Edwin Swalle
|
Na Veronica Mwafisi-Mwanza
Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imepongezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa kutekeleza Mradi wa Zahanati katika eneo lenye changamoto ya miundombinu na kuokoa maisha ya wakazi wa eneo hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 16 Machi, 2026 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Akizungumza kwa niaba ya kamati yake, Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema ujenzi wa zahanati hiyo ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Mihama na Kata ya Kitangiri ambao ilikuwa ni changamoto kutoka katika eneo hilo kutafuta huduma sehemu nyingine.
Kwa changamoto ya kufika huku, niwapongeze TASAF kwa kutekeleza mradi huu katika eneo hili kwani itaokoa maisha ya wananchi wa eneo hili na gharama walizokuwa wakitumia kufuata huduma za matibabu katika eneo lingine. Ameongeza.
Mhe. Ndumbaro ameongeza kuwa maendeleo haya ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambacho kimekusudia kuwajali wananchi wake kwa kuwapa huduma mbalimbali ikiwemo za kijamii.
Aidha, ametoa wito kwa uongozi wa Halmashauri hiyo ya Ilemela kuhakikisha zahanati hiyo inawekwa chini ya Halmashauri hiyo. TASAF imetekeleza, zahanati hii ni ya kwenu sasa, mfanye utaratibu iwe chini ya Halmashauri, amesisitiza Mhe. Dkt. Ndumbaro.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema zahanati ya Mihama ni sehemu ya vielelezo vya miradi inayotekelezwa na TASAF kwa lengo la kuwahudumia wananchi.
Mhe. Kikwete amewataka wananchi wa Mihama na Kitangiri kuitunza zahanati hiyo ili iweze kuwahudumia kama ilivyokusudiwa.
Ameongeza kuwa, katika kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kikamilifu, katika ajira 12,000 zilizotolewa na Serikali ndani ya siku 100, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemelea imepewa watumishi wa afya 37 na elimu 40.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TASAF, Bw. Shadrack Mziray ameishukuru Kamati kwa kuitembelea zahanati hiyo na kushuhudia maendeleo yaliyofanywa na Serikali katika eneo hilo.
Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wananchi wa eneo la Mihama, Bi. Mary Nyanda ameishukuru Serikali kwa kujenga zahanati katika eneo hilo kwani walikuwa na uhitaji mkubwa wa zahanati.
Zahanati hii ni mkombozi kwetu watu wa Mihama, kwa miaka 25 tumekuwa tukihangaika kufuata huduma sehemu nyingine, tunaishukuru sana Serikali kwa kutekeleza hili, ameongeza Bi. Nyanda.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, imehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Geita na jijini Mwanza
No comments:
Post a Comment