Mwili
wa aliyekuwa spika wa bunge, Samuel Sitta unatarajia kuwasili nchini
siku ya Alhamis ukitokea nchini Ujerumani ambapo alipokuwa akipatiwa
matibabu.
Taarifa hiyo imetolewa na Gerald Mongela ambaye ni msemaji wa familia.
Amesema
mara baada ya mwili huo kuwasili nchini utapelekwa nyumbani kwa
marehemu Masaki jijini Dar es Salaam na siku ya Ijumaa shughuli za kuaga
zitafanyika katika viwanja vya Karimjee kisha kupelekwa bungeni mjini
Dodoma.
“Mwili
wa mpendwa wetu mheshimiwa Samuel Sitta utawasili na ndege ya Emirates
siku ya Alhamis saa tisa na nusu alasiri na baada ya hapo mwili
tutauleta hapa nyumbani kwaajili ya kukaa nao na kupumzika kusubiri
ratiba ya Ijumaa,”alisema Mongela.
Mazishi ya Marehemu Samwel John Sitta yatafanyika siku ya Jumamosi Urambo mkoani Tabora.
No comments:
Post a Comment