Serikali
ya Tanzania imesema kwamba kulingana na takwimu inaonesha kuwa ukosefu
wa ajira kwa vijana nchini Tanzania umepungua kwa asilimia mbili,
kutoka asilimia 13.7 mwaka 2012 mpaka asilimia 11.7 mwaka huu.
Akizungumza jana
bungeni, mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe.
Anthony Mavunde, alisema
licha ya kupungua huko kwa ukosefu wa ajira, serikali imeweka mipango
ya kuwawezesha vijana kuwa na wigo mpana wa ajira nchini.
Mhe. Mavunde alisema
kuwa kwa takwimu hizo Tanzania ni nchi inayoongoza kwa kutoa ajira kwa
vijana wengi zaidi kushinda baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo
Kenya na Uganda.
No comments:
Post a Comment