NEYMAR-MESSI USO KWA USO, BRAZIL KUFUTA KIPONDO KILICHOBATIZWA 'MINEIRAZO'?
UWANJA wa Mineirao huko Mjini Belo Horizonte daima utabaki na kumbukumbu ya uchungu kwa Taifa la Brazil kwani huko ndiko walikopigwa 7-1 na Germany kwenye Mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia Mwaka 2014.
Mineirao Stadium ipo Kaskazini ya Brazil Kilomita 250 toka Rio De Janeiro na Alhamisi Usiku Watu 62000 watasheheni ndani yake kuishuhudia Brazil ikicheza na Mahasimu wao wakubwa Argentina kwenye Mechi ya Kanda yacNchi za Marekani ya Kusini ya kusakefa kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Wabrazil wanataka sana kuifunga Argentina ili kufuta machungu ya kisago cha Germany na pia kuzidi kupaa kileleni mwa Kundi hili ambalo wanaongoza baada ya Mechi 10 wakiwa Pointi 5 mbele ya Argentina walio Nafasi ya 6.
Akiongea kuhusu Mechi hii na hasa kuchezea Mineirao, Kocha wa Brazil, Tite, ameeleza: "Ni kweli kurejea hapa kunatugusa wote hara wale ambao hawakucheza na Germany. Miaka Miwili imepita na tuko tofauti!"
Tangu Tite atwae mikoba, Brazil imeshinda Mechi zao zote 4.
++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-CONMEBOL itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.
-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5
kwenye Kundi lao itashinda Mechi ya Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka
Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za
Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea,
Solomon Islands na Tahiti.
++++++++++++++++++++++++
Wachezaji Watatu wa Brazil ambao walicheza Mechi hiyo na Germany na wanatarajiwa kucheza na Argentina ni Fulbeki w Real Madrid Marcelo, Kiungo wa Manchester City Fernandinho na Kiungo wa Guangzhou Evergrande Paulinho.
Akiongea kuhusu Mechi hii Paulinho ameeleza: "Brazil ina nafasi kuandika nafasi mpya. Hatuwezi kubadili kilichotokea lakini tunaweza kuleta matokeo bora! Hii ni nafasi safi dhidi ya Timu Bora!"
Wakati Brazil wakihaha kufuta Jinamizi la 2014 ambalo huko kwao
limebatizwa Jina "MINEIRAZO", Argentina wana kiherehere cha kuogopa
kutofuzu kwenda Russia 2018.
Kocha wa Argentina Edgardo Bauz amekiri wasiwasi wao wa kutofuzu na hasa kuikabili Timu ngumu Brazil na kisha Jumanne Novemba 15 kuvaa kigaga kingine Colombia.
Hii ni Mechi spesho ikikumbusha Mineirazo na pia ikikutanisha Mahasimu wa Jadi lakini pia mvuto mkubwa ni kukutana uso kwa uso kwa Mastaa wa Klabu ya FC Barcelona, Neymar Kepteni wa Brazil.na Lionel Messi Kepteni wa Argentina.
MSIMAMO:
CONMEBOL
Kombe la Dunia – Russia 2018
Mechi za Makundi
Ratiba:
**Saa za Bongo
CONMEBOL
Alhamisi Novemba 10
2330 Colombia v Chile
Ijumaa Novemba 11
0200 Uruguay v Ecuador
0230 Paraguay v Peru
0230 Venezuela v Bolivia
0245 Brazil v Argentina
Jumanne Novemba 15
2300 Bolivia v Paraguay
Jumatano Novemba 16
0001 Ecuador v Venezuela
0230 Argentina v Colombia
0230 Chile v Uruguay
0515 Peru v Brazil
No comments:
Post a Comment